Breaking News. Mkurugenzi mkuu Taasisi ya Elimu atumbuliwa

Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amemteua ndugu Stafford P. Mwakipesile, kuwa mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania. Hii inafuatia kutokana na kuondolewa kwa aliyekuwa mkurugenzi wa taasi hiyo ndugu Dk Paul Mushi Kutokana na kukumbwa na kashfa ya kasoro au madudu yaliyo jitokeza katika vitabu vya kufundishia vya kiingereza na katika syllabus za masomo mbalimbali kwa mujibu wa kurugenzi la mawasiliano Ikulu iliyotolewa leo jumapili. Taarifa zaidi zitakujia hapo Kesho.